Luke 18:18-23

18 a bMtawala mmoja akamuuliza Isa, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

19Isa akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna yeyote aliye mwema ila Mungu peke yake. 20 cUnazijua amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.’ ”

21Akajibu, “Amri hizi zote nimezishika tangu nikiwa mtoto.”

22 dIsa aliposikia haya, akamwambia, “Bado kuna jambo moja ulilopungukiwa. Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

23Aliposikia jambo hili, alisikitika sana kwa maana alikuwa mtu mwenye mali nyingi.
Copyright information for SwhKC